Kanuni za ulinzi wa data
- Grace Bomu and Oliver Ochieng |
- May 12, 2020 |
- Data Protection,
- Information Technology,
- RIght to data protection,
- Tech-Legislation
a) faragha
Kila anayekusanya au kutumia data binafsi lazima azingatie faragha/usiri wa mwenye data.
b) sheria
Kila anayekusanya au kutumia data binafsi anapaswa kuzingatia usheria, usawa nauwazi anapochakatua data hiyo.
c) madhumuni
Data binafsi lazima ikusanywe kwa madhumuni maalum na kwa malengo halali na isitumike kinyume cha na madhumuni hayo.
d) kupunguza
Data binafsi ikusanywe kulingana na madhumuni ya utumizi wake na isizidi madhumuni yake.
e) ufafanuzi
Wanaokusanya data binafsi lazima watoe maelezo halali wakati wowote data kuhusu familia au mambo ya kifaragha yanahitajika.
f) sahihi
Kila hatua ichukuliwe kuhakikisha kwamba data binafsi inayokusanywa na kutumika ni sahihi, na inasasishwa au kusahihishwa bila kupoteza muda.
g) uhifadhi
Data binafsi isiwekwe kwa muundo unaomtambulisha mwenye data wakati madhumuni ya kukusanya data hiyo yamekamilika.
h) uhamisho nje ya nchi
Data binafsi isihamishwe nje ya nchi ya Kenya bila dhibitisho kwamba nchi hiyo nyingine ina sera sambamba za kutosha ulinzi wa data binafsi, au kwa ruhusa ya mwenye data.