USANII NA SANAA: JINSI YA KULINDA SANAA YAKO

USANII NA SANAA: JINSI YA KULINDA SANAA YAKO

Akili ni nywele, na kila mja ana zake.

Katika uandishi wa hapo awali, tuliangazia maana ya ‘mali ya akili’ na ‘haki miliki’; kisha tukaelezea umuhimu wa mali hii na umuhimu wa kuilinda. Tuliashiria kuwa mali hii huchukua mifano mitatu kuu.
Katika uandishi wa leo, lengo litakuwa kujadili mfano wa sanaa na jinsi wasanii wanaweza kulinda kazi zao za kisanaa.

Sanaa huwa umetuzingiria kila pahali; mara nyingi huchukua mfano wa vitabu tunavyo visoma, nyimbo tunazoskiza, vipindi tunavotazama kwa runinga na mifano mingineyo. Nchini Kenya, kazi hizi za kisanaa hulindiwa na sheria iitwayo Copyright Act, No. 12 of 2001.

Sheria hii inaashiria na kutafsiri ni kazi zipi za kisanaa ambazo hulindwa, jinsi ya kulinda kazi hizi, na haki mmiliki wa kazi hii hupata.

Kulingana na kifungu cha ishirini na mbili (22) cha sheria hii, kazi zinazostahiki ulizi ni kazi za uandishi, kazi za kimuziki, kazi za kisanii (uchoraji), michezo ya kuigiza, kazi ambazo ni za kuona kwa sauti, rekodi za sauti na kazi zinazo tangazwa kwenye vyombo vya habari.

Kazi hizi lazima ziwe asili, ziwe katika fomu inayoonekana na kutumika, na lazima bidii kiasi iwe imewekwa ili kuipa kazi hiyo uasili wake. Pasipo kufikia malengo haya tatu, kazi yoyote ya kisanaa haiwezi fuzu kupata ulinzi.

Ulinzi wa kazi za sanaa humpa mmliki wa ulinzi huu haki mbili kuu; haki za kiuchumi na haki za kimaadili. Haki za kiuchumi humwezesha mmliki wa haki hizi kutumia kazi ya kwa njia tofauti zenye zinaweza kumpa pesa. Chini ya haki za kiuchumi, mmliki wa haki hizi anaweza, kutoa nakala na kuzalisha tena kazi yake, kutafsiri kazi yake, kusambaza kazi yake hadharani na pia kutangaza kazi ya kwa umati. Haki hizi, ni muhumu kujua zinaweza kuuuzwa na umulikaji kupitishwa kutoka mtu mmoja au mwingine, sanasana kwa njia ya leseni.

Kwa upande mwingine, haki za kimaadili humpa mmliki haki ya kudai ndiye muumba wa kazi yake na nafasi ya kupinga uharibifu na kudhrauliwa kwa kazi yake. Haki hii haswa haiwezi uzwa au umiliki wake kupitishwa kwa mtu mwingine kwa soko huru. Haki hii hupita tu baada ya kifo cha mmiliki au kufuatia amri ya Korti.

Kulingana na sehemu 22(5) ya Copyrights Act, haki hizi hutoshelezwa moja kwa moja kazi inapotolewa katika fomu inayoonekana na kutumika. Hata hivyo, hii si kinga tosha; kwani mmiliki akihitaji kuthibitisha umiliki wake, lazima atoe cheti cha usajili. Hii ndio umuhimu wa kusajili kazi.

Mwisho, mara kwa mara haki hizi hukiukwa na watu bila ruhusa ya mmiliki wa haki hizo. Mkiukaji wa haki hizi, kulingana na sehemu 35(4) ya Copyright Act, anaweza kuletwa mbele ya korti kujibu mashtaka. Hata hivyo, si ukiukaji wote ambao unakatazwa na sheria. Ratiba ya pili ya Copyright Act inaangazia wakati ambapo ukiukaji wa haki hizi unakubaliwa; inajumuisha matumizi ya kazi hizi masomoni, matumizi katika maktaba na matumizi mengine ya kijumla.

Kwa hivyo, kama msanii, ni muhumu kujua kuwa kunasheria ambayo inalinda usanii. Ni muhimu kuisajili kazi mpya ikiundwa ili kuchunga isitumike kwa njia itakayo kugharimu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked