Ni nini maana ya Mali ya Akili na Haki Miliki?

Ni nini maana ya Mali ya Akili na Haki Miliki?

Kama wanadamu, akili zetu hujawa na mawazo ya jinsi ya kusuluhisha shida zilizopo katika maisha yetu. Mawazo haya yanaweza kuzaa teknologia na mengine kuegemea katika dunia ya sanaa; kama vile nyimbo, vitabu na michezo za kuigiza.

Katika wiki zijazo, lengo letu litakuwa kukuelezea zaidi kuhusu kazi ambazo hutokana na mawazo yetu, na jinsi uvumbuzi tofauti unaotokana na mawazo haya hulindwa na sheria.

Katika uandishi wa leo, tutaelezea kwa upana maana ya ‘mali ya akili yako’, ‘haki miliki’ na umuhimu wa kuilinda.

Ni nini maana ya “Mali ya Akili Yangu?”

Kama vile jina linaashiria, mali ya akili ya mtu ni uzao au kitu chenye thamani kinacho tokana na wazo la mtu. Kwa lugha ya Kingereza ni “Intellectual Property”. Mali hii huchukua mifano tatu kuu;

  1. Sanaa – hii, kwa jumla, huwa ni mitungo bunifu, kwa mfano nyimbo, vitabu, sinema na mengineyo.
  2. Teknolijia mpya na vyombo vya viwanda – mfano huu huangalia mashine na njia buni za kusuluhisha shida za kiteknolojia, na pia kuziboresha. Mifano ni kama jokofu na michakato buni na bora ya kutengeneza vitu tofauti.
  3. Alama ya biashara – hii ni saini maalum inayo tofautisha bidhaa moja kwa nyingine sokoni. Kwa mfano, kinywaji cha Coca-Cola hutofoutishwa na vinywaji vinginge kwa kutumia alama yake maalum.

Zipo sheria ambazo hulinda aina hizi tofauti za uvumbuzi na hujulikana kama haki miliki. Sheria hizi humpa mbunifu haki za kuukinga ubunifu wake dhidi ya wizi, kwa muda maalum. Hivyo basi, haki hizi husajiliwa na kutekelezwa na mtu binafsi, wala si na serikali. Kwa hivyo, ni muhimu kujua kuwa ili kuweza kutekeleza haki zako, lazima kwanza usajili kazi yako pafaapo.

Isitoshe, haki hizi hutekelezwa nchini ambapo zimesajiliwa, pekee yake; na si dhidi ya dunia nzima. Kwa mfano, kazi buni ikisajiliwa nchini Kenya, mmiliki wa haki hizi hawezi kuzitekeleza nchini Tanzania au kwingine, isipokuwa Kenya pekee yake. Akitaka kulinda kazi yake buni katika nchi nyingine, lazima asajili ubunifu wake nchini mle.

 

Ni nini umuhimu wa Haki Miliki?

Kunazo sababu nyingi za kulinda mali na kazi zilizotokana na mawazo yako; baadhi ya sababu hizi ni:

  1. Huendeleza uvumbizi wa teknolojia mpya, ambazo hurahisisha kazi za kila siku.
  2. Huchangia katika ukuuzaji wa sanaa na talanta.
  3. Huchangia katika kuenea kwa uchumi wa nchi yetu.
  4. Kama mmiliki wa mali hii, unaweza pata riziki.
  5. Kibiashara, huchochea viwanda kufanyaa bidii ili kuwapa wateja wao vifaa na bidhaa za hali ya juu.

Katika uandishi ufuatao, tutangalia kwa makini jinsi sanaa hulindwa na haki zinazoambatana na ulinzi huu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked